Ili kuzuia ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona watu nchini Mauritius kuanza sasa wanatakiwa kwenda madukani katika siku maalum na kwa kuzingatia herufi za mwanzo za majina yao ya  ukoo.

 

Waziri Mkuu wa nchi hiyo Pravind Jugnauth amesema hatua hii itapunguza msongamano wa watu na kusema wanunuzi wataofika kununua bidhaa watatakiwa kutumia muda wa nusu saa peke yake kumaliza kununua bidhaa.

 

Aidha ratiba iliyotolewa inasema  wenye majina ya ukoo kuanzia A- hadi -F watakwenda madukani siku za Jumatatu na Alhamisi, G hadi N wataenda siku ya Jumanne na Ijumaa na O hadi Z wataenda siku za Jumatano na Jumamosi. huku Maduka yote yakitakiwa kufungwa siku ya Jumapili.

 

Mpaka sasa nchi hiyo imeripoti vifo 7 vinatokana na virusi hivyo na watu 161 wakiripotiwa kuugua COVID-19

Share with Others