Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na watoto Ummy Mwalimu ametangaza ongezeko zaidi la wagonjwa wa Corona na kufikia watatu huku washukiwa 27 wa ugonjwa huo mkoa wa Arusha wakiwekwa kwenye Karantini na sampuli zao zikipelekwa maabara ya Taifa.

Akiongea na vyombo vya Habari jijini Arusha, Waziri Ummy amesema ongezeko hilo limetokana na washukiwa wawili ambao ni mwanaume raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 61 mkazi wa Dar es salaam kukutwa na maambukizo ya Corona.

Amemtaja mwanaume mwingine kutoka Zanzibar mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ujerumani kukutwa na maambukizi ya Corona baada ya Sampuli zao kupelekwa kwenye maabara ya Taifa na kubainika kuwa wana virusi vya Corona.

Aidha amesema kuwa mgongwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na ugonjwa wa Corona hapa nchini ambapo waziri Ummy alimtangaza Marchi 16 mwaka huu, Mwanamke Hugo mwenye umri wa miaka 46 amedai kuwa anaendelea vizuri kiafya.

Waziri Ummy ambaye aliongea na mgonjwa huyo kwa njia ya Simu wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Arusha,mgonjwa huyo mwanamke amesikika akisema kuwa maendeleo yake ni mazuri na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu juu ya Afya yake huku akiomba radhi watanzania kwa kuwaletea corona

Katika hatua nyingine waziri Ummy amewaeleza wanahabari kwamba jumla ya washukiwa 27 wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona Mkoa wa Arusha wamewekwa kwenye Karantini wakisubiri hatima yao baada ya sampili zao kupelekwa maabara ya taifa

Naye Mkurugenzi msaidizi kitengo cha Milipuko kutoka wizara ya Afya ,dkt Janeth Mghaba ameeleza njia sahihi ya kujikinga na maambukizi ya Corona kuwa no pamoja na kuepuka mikusanyiko ikiwemo kutosogeleana umbali wa mita moja.

 

Ameongeza kwamba uvaaji wa Maksi mdomoni kuwa anayetakiwa kutumia kinga hiyo ni mtu mwenye maambikizo pekee ya Corona na mhudumu wa Afya ili kuepusha kumwamwambukiza MTU mwingine huku akisisitiza kuwa vifaa hivyo vitumike ndani ya Massa manne tu na kuvibadilisha na sio vinginevyo.

 

Amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata naelekezo ya kitaalamu yanayotolewa na wataalamu wa Afya namna ya kujikinga na maambikizi ya Corona ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kila wakati,kutoshikana mikono wakati wa kusalimiana na kwamba ugonjwa huo unaambukiza kwa njia ya majimaji na hewa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa onyo Kali kwa baadhi ya wamiliki wa shule ambao amepata taarifa kuwa bado wanaendelea kufundisha wanafunzi kwa siri ,kinyume na maelekezo ya serikali kuwa, shule hizo zikibainika zitachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Gambo amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo na lazima na wenye magari ya kusafirisha abiria kuepuka kujaza kupita kiasi.

Share with Others