Tetemeko kubwa lililopiga  kisiwa cha Hokkaido, kaskazini mwa Japani limeua watu 44 na hakuna mtu ambaye alitoweka, serikali imetangaza hivyo.
Takribani waokoaji 40,000 (maafisa wa Zima Moto, polisi, askari) wamekua wakiendelea kutoa msaada kwa wakazi wa kisiwa hicho, ambapo zaidi ya watu 2,700 wameyahama makaazi yao.
Vifo vingi vimeripotiwa katika kijiji cha Atsuma, ambako nyumba zilifunikwa kwa matope kutokana na tetemeko lenye ukubwa wa 6.6 katika vipimo vya Richter.
Waziri Mkuu Shinzo Abe, ambaye alizuru siku ya Jumapili eneo hilo lililokumbwa na tetemeko la ardhi, aliahidi kufanya kilio chini ya uwezo wake ili kurekebisha maeneo yaliyoathirika na majanga ya asili ya hivi karibuni.
Kabla ya tetemeko hilo la ardhi la Hokkaido, eneo la magharibi ya nchi lilipigwa na dhoruba kali ambayo iliua watu 11 na kusababisha kufungwa kwa uwanja wa ndege wa Kansai (Osaka).
 

Share with Others