Zaidi ya watu 400 wamejitokeaza kufanyiwa upasuaji wa mabusha kati ya watu 170 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Lindi Sokoine.


Hayo yameelezwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt GENCHWELE MAKENGE alipokuwa akizungumza na Mashujaa Fm kuhusu zoezi hilo ambalo linafanywa bure na timu ya madaktari kutoka muhimbili, Wizara ya Afya kwa ufadhiri wa kampuni ya Equanor.


Baadhi ya waliojitokeza kufanyiwa upasuaji huo wameshukuru kwa kupatiwa huduma hiyo kwani wengi wao wamekuwa wakishindwa kupata matibabu yake kutokana na kuwa na kipato kidogo.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi SHAIBU NDEMANGA amesema serikali itaendelea kuwasaidia wananchi wake katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za afya na ametoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kuikutoiacha fursa hiyo ya upasuaji ambayo imewaondolea ghalama.


Kwa mujibu wa mganga mkuu Dkt GENCHWELE hiyo ni awamu ya nne ya upasuaji,na kwa awamu ya kwanza walifanyiwa upasuaji wagonjwa 200,ya pili wagonjwa 218 huku awamu ya tatu wakifanyiwa wagonjwa 150.

Share with Others