Shirika la Save the Children limeonya kuwa watu milioni 33 kutoka nchi kumi za Afrika Mashariki na Kusini wako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika hilo limetoa ripoti hiyo katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (COP25) uliofunguliwa jana huko Madrid, Hispania ambapo limesema kuwa eneo hilo lina watu milioni 162 wenye umri wa chini ya miaka 18, huku zaidi ya watoto milioni 16 wako "katika shida au kiwango cha dharura cha njaa."

Pamoja na hayo shirika hilo liliendelea kuonya kuwa nchi ya Afrika Kusini ina joto mara mbili zaidi ya kiwango cha ulimwengu na nchi nyingi zimepigwa na mshtuko wa hali ya hewa hiyo, pamoja na Msumbiji, ambayo iliona vimbunga vikali vikali katika msimu huo huo kwa mara ya kwanza katika historia.

Ripoti imeongeza kuwa mwaka huu baadhi ya sehemu za Mashariki na Kusini Barani Afrika zilikumbwa na mafuriko, maporomoko ya udongo, ukame na vimbunga, zaidi ya watu milioni 33 wako kwenye hali ya dharura ya ukosefu wa chakula au hali mbaya zaidi

Share with Others