Kwa mjibu wa shirika la Madaktari wasio na Mipaka MSF. Watu zaidi ya mia moja, ikiwa ni pamoja na watoto ishirini, wamekufa maji baada ya boti mbili walizokuwemo kuzama katika pwani ya Libya mapema mwezi Septemba.
Mashahidi waliohojiwa na wafanyakazi wa MSF, wamesema boti mbili ziliondoka pwani ya Libya Septemba 1 , na kila boti ilikua imebeba watu 160, kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo lisilo la kiserikali.
Ambapo ripoti ikisema katika boti hizo kulikuwa na raia kutoka Sudan, Mali, Nigeria, Cameroon, Ghana, Libya, Algeria na Misri. Boti moja lililokua limebeba watu 165 , ikiwa ni pamoja na watoto 20 lilipatwa na tatizo la injini na kuanza kuzama, huku watu  wachache tu wakiweza kuokolewa.
Ripoti zimeendelea kusema kwamba Watu 55 pekee ndio walinusurika huku Watoto zaidi ya 20 wakifariki, kulingana na chanzo hicho, kilichonukuliwa na MSF.
Waathirika ni pamoja na wanawake wajawazito, watoto, na watoto wachanga, MSF imeongeza.

Share with Others