Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo amezindua ripoti ya utafiti wa kiwango cha matumizi ya Tumbaku kwa watu wazima. Taarifa hiyo inahusisha tathmini ya matumizi, watu waliojaribu kuacha, gharama za matumizi, ufikiwaji wa taarifa za madhara

Amesema Taarifa inaonesha kuwa watu 4 kati ya 10 (32.9%) wameathiriwa na moshi wa tumbaku sehemu za kazi ikiongozwa na sehemu za mabaa na kumbi za starehe kwa 77% sawa na watu milioni 3, maeneo ya biashara za vyakula 31.1% na majumbani 13.8%

Aidha, mtu 1 kati ya 10 (8.7%) wenye umri wa miaka 15 au zaidi wanatumia Tumbaku. Hivyo watu milioni 2.6 nchini wanatumia Tumbaku ikiwa ni Wanaume 14.6% na Wanawake 3.2%

"Katika utafiti wa matumizi ya tumbaku kwa watu wazima wa mwaka 2018, mtu mmoja kati ya wawili (48.4%) wanaotumia tumbaku nchini alishawahi kujaribu kuacha, aidha wastani wa matumizi ya tumbaku kwa mtu mmoja kwa mwezi inagharimu Tsh. 28,840"

Amesema Tanzania kama nchi nyingine za Kiafrika wavutaji wa Tumbaku wako hatarini kuyumba kiuchumi na kupata magonjwa yasiyoambukizwa kama tahadhari hazitachukuliwa mapema

Share with Others