Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amesema Kaulimbiu ya “Mshahara Wangu Upo Wapi” ambayo imeandaliwa na Mkoa, itamlazimu kila Mtumishi wa Serikali kuonesha mafanikio aliyopata kutokana na Mshahara anaolipwa ifikapo mwisho wa mwaka

Dkt. Nchimbi amesema, lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mishahara inatumika kuboresha Uchumi na kuleta tija katika familia

Amewataka watumishi kufanya kazi na kuacha Siasa, huku akionya kuwa watumishi wazembe wataondolewa mara moja ili kuwaachia nafasi kwa wale wanaoendana na Kaulimbiu ya "Hapa Kazi Tu" ya serikali ya awamu ya Tano 

Mkoa wa Singida umeamua kuwa na kaulimbiu hiyo baada ya kuona mafanikio makubwa waliyopata wanufaika wa mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ulioanzishwa rasmi mkoani humo Septemba 2014

Pamoja na hayo, Dkt. Nchimbi amesema Mkoa wa Singida pia umejipanga kufanya Kilimo cha Kisasa na kutoa wito kwa Wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili waweze kupewa maeneo na kuyaendeleza

Share with Others