Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema, Serikali itawasaka Wazazi takriban 17,000 ambao watoto wao hawajaripoti shuleni kwa ajili ya masomo ya Kidato cha Kwanza yaliyoanza rasmi wiki tatu zilizopita

Byanakwa amechukua hatua hiyo baada ya kufanya ziara Manispaa ya Mtwara Mikindani na kukuta Wanafunzi zaidi ya 3,000 bado hawajaripoti shuleni

Inaelezwa kuwa, Wanafunzi 20,400 walifaulu mitihani ya Darasa la Saba na walitakiwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu lakini hadi sasa, asilimia 75 ya Wanafunzi hao bado hawajaripoti Shuleni

Mkuu huyo wa Mkoa amesema, itakapofika Jumatatu, Wazazi ambao wamegoma kupeleka watoto wao shuleni watachukuliwa hatua za kisheria huku akisisitiza kuwa, hali hiyo haivumiliki

Ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vijiji, Vitongoji na Mitaa kuhakikisha Wazazi hao wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani

Share with Others