Waziri Mkuu wa Finland Sanna Marin, amependekeza Nchi hiyo kuwa na Siku Nne (4) za kufanya kazi ili wananchi wawe na fursa ya kuwa na familia zao kwa muda mrefu zaidi na kufanya mambo mengine ya jamii ikiwemo michezo na utamaduni.

Pamoja na pendekezo hilo, Marin pia amependekeza muda wa kazi kupunguzwa kutoka Saa Nane (8) hadi Sita (6) kwa siku ili wananchi waweze kufanya shughuli nyingine za Kijamii 


Alinukuliwa akisema, “Naamini Wananchi wana haki ya kutumia muda wao mwingi na familia zao, wapenzi wao na mambo mengine katika maisha kama vile 'Hobby' na Utamaduni. Hii itakuwa hatua kubwa kwetu katika Maisha ya kazi”

Aidha, Waziri wa Elimu wa Nchi hiyo Li Andersson, ameunga mkono hoja ya Marin na kudai kuna umuhimu mkubwa wa kuruhusu Raia kufanya kazi kwa kiasi

 

Hivi sasa Nchi ya Finland ina utaratibu wa kufanya kazi kwa Saa Nane (8) kwa Siku, na Siku Tano (5) kwa Wiki

Share with Others