Waziri wa Kazi nchini Uganda, Mwesigwa Rukutana anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo pamoja na walinzi wake watatu kwa kujaribu kuua.

Polisi nchini Uganda imemkamata na kumuweka mahabusu Naibu waziri wa kazi nchini humo Mwesigwa Rukutana kufuatia tukio ufyatuaji wa risasi katika eneo la Ruhama wilayani Ntungamo, ambapo mtu mmoja ameuawa.

Waziri Mwesigwa Rukutana amekamatwa na jeshi la polisi baada ya picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa zilizoonesha akichukua silaha kwa mlinzi wake na kuwafyatulia risasi dhidi ya wampinzani wake.

Risasi hizo ziliangukia kichwani Dan Rwiburingi ambaye inayesemakana amefariki dunia siku hiyo hiyo alipokua akipata matibabu hospitalini.

Picha kadhaa pia zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya ijumaa zikionesha Bwana Rukutana akishikilia bunduki. Pia kuna picha zinazoonesha muathiriwa wa shambulio hilo:

Tukio hilo lilitokea wakati wa kampeni za kuwania kiti cha ubunge jimbo la Rusheni wilayani Ntugamo magharibi mwa Uganda kwa tiketi ya chama tawala cha NRM.

Kulingana na Matokeo yaliyotolewa siku ya Ijumaa wilayani waziri Rukutana alipoteza kiti cha ubunge ambacho kilichukuliwa na mpinzani wake Naome Kabasharira.

Katika uchaguzi huo zaidi ya mawaziri 10 katika serikali ya rais Museveni wamepoteza viti katika kura za mchujo wa chama, ambapo kampeni za uchaguzi huo zimekua zikigubikwa na ghasia, vitisho na rushwa kwa wapiga kura.

 

Share with Others