Takriban watoto 2200 hadi 3000 wanazaliwa na tatizo la mguu kifundo yani nyazo zilizopinda kila mwaka nchini, huku hospitali ya CCBRT ikipokea watoto na watu wazima 400 wenye tatizo hilo kila mwaka.


Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na daktari wa Mifupa Dkt Zainabu Illonga kutoka hospitali ya CCBRT kwenye maadhimisho ya siku ya mkuu kifundo duniani (World club foot day) na kuishauri jamii kuwapeleka watoto wenye tatizo hilo hosptali ili kupatiwa matibabu.

Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa CCBRT Brenda Msangi amesema kutokana na changamoto ya gharama, hospitali imeamua kutoa huduma ya matibabu bure kwa watoto wenye miguu vifundo, huku pia ikiongeza muda wa kazi kwa kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona.

Kwa upande wao akina mama ambao watoto wao wanapatiwa huduma ya matubabu ya mguu kifundo, wamesema wanafurahishwa na huduma za hospitali hiyo huku wakiwashauri wawazi wengine wenye watoto wenye tatizo hilo kuwapeleka hospitali.

Kila Juni 3 huwa ni siku ya mguu kifundo duniani au nyayo zilizopinda (World club foot day) ambapo kitaifa imefanyika katika hosptali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar es salaam

 

Share with Others