Waandamanaji wenye hasira kali wameuzingira mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa baada ya kuuawa kwa watu 23 wakati wa mapigano ya kikabila yaliyoibuka mwishoni mwa juma lililopita.
Wamezuia barabara kuu za jiji hilo, sambamba na kufunga biashara mbalimbali wakiitaka serikali ichukue hatua muhimu kuzuia mauaji hayo.
Wakaazi wa jiji hilo wanawalaumu vijana wa kabila la Oromo kuwa walianzisha fujo katika mitaa ya mji wa Burayu ambapo walitumia visu, mawe na vyuma.
Mkuu wa polisi katika Jimbo la Oromo, Alemayehu Ejigu, akinukuliwa na ENA, amesema kuwa kundi lililokuwa limejiandaa liliendesha mfululizo wa mauaji na uporaji kuho Burayu, magharibi mwa Addis Ababa, na kuua watu 23 na kusababisha watu 886 kuyatoroka makazi yao.
vikosi vya usalama vilitumwa ili kuzuia hali isiendelei kuzorota zaidi, huku watuhumiwa 70 wakikamatwa, 
 

Share with Others