Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kitengo cha Elimu ya Afya inaendelea na zoezi la uelimishaji kwa Umma juu ya namna mbalimbali za kujikinga na ugonjwa wa COVID-19 katika maeneo tofauti ya Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi 

Zoezi hilo linatoa hamasa kwa Wananchi juu ya kuufahamu Ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona na kutambua namna ya kujikinga.

Wananchi katika Maeneo tofauti ya Manispaa ya Lindi wamehudhuria kampeni hiyo na kutatuliwa maswali yao juu ya Ugonjwa huo 

Sambamba na hilo Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Genchwele Makenge amewataka Wananchi kwenda na kasi ya uchumi wa kati kwa kujenga Vyoo bora ili kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwemo magonjwa ya tumbo na magonjwa mengine hatarishi.

'Halmashauri ya Manispaa ya Lindi bado inakabiriwa na changamoto ya Wananchi kutokuwa na Vyoo bora na kaya nyingine kukosa vyoo kabisa nakutumia vichaka vya porini kama sehemu za kujikidhi haja' DKT. Makenge

Aidha Dkt. Makenge amesema kuwa ataanza kutumia sheria na kuwatia nguvuni wale wanaokaidi agizo la serikali la kuwa na vyoo bora na kutoa 60 kuanzia 22 Julai 2020 kwa wakazi wa Kijiji cha Kineng'ene kuhakikisha wanakuwa na vyoo vyenye ubora.

Uhamasishaji huo wa corona unatarajia kuvifikia Vijiji zaidi ya 130 na Vituo vya Afya 103 katika Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi 

Share with Others