Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya mashine inayotumika kuchemshia korosho kulipuka wakati wakipatiwa mafunzo ya ubanguaji korosho yanayotolewa na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO mkoa wa Lindi.

 

Akithibitisha kupokea mwili wa marehemu na majeruhi hao, Katibu wa afya hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine, BONIFACE LYMO amemtaja aliyefariki kuwa ni SAADA JUMA ISSA (28) mkazi wa Msinjaili ambaye alijeruhiwa vibaya sehemu za shingoni ni kitu chenye ncha kali.

 

LYMO amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospital hiyo.

Amesema waliojeruhiwa ni Aisha Mohamed  ambaye ameruhusiwa baada ya kupatiwa huduma na Amedeus Joseph ambaye amelazwa katika hospitali hiyo akiendelea kupatiwa matibabu.

 

Akizungumza na mashujaa Fm hospitalini hapo wakati akiendelea kupatiwa matibabu, AMEDEUS amesema tukio hilo limetokea wakati wakiendelea na Semina ya ubanguaji korosho.

 

Share with Others