Akizungumza na East Africa Television kupitia DADAZ inayorushwa mubashara kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 5 Asubuhi, Dkt Ellie amesema kuwa mwanamke siku zote hana imani kama anapendwa na tegemeo kuu la mwanamke  ni furaha, na si upendo kama watu wengi wanavyofikiri.

“Mwanamke ana mapenzi ila hana upendo, mwanamke hapendi bure bali anapenda kwa mazao, na zao kuu analolitegemea ni furaha na kicheko. Mwanamke anapenda maneno mengi mazuri ndiyo maana anaongea zaidi ya maneno 25,000 'maximum' kwa siku,na mwanaume 'maximum' yake ni maneno 12,500”. Amesema Dkt. Ellie

Aidha, Dkt Ellie ameongeza kuwa katika mapenzi au upendo  suala la mazoea ni moja ya chanzo cha migogoro katika mahusiano na njia kuu ya kuepuka migogoro ni kuwepo umbali kati ya wapenzi hata kwa muda mfupi wa masaa kadhaa kwa siku na pia kuwepo kujali na kuthaminiana.

Pia kulingana na utafiti wa Daktari na Mshauri  wa Masuala ya Ndoa na Mwakilishi kutoka  taasisi 'BEST LIFE' ya Newyork  nchini Marekani, imeelezwa kuwa mwanamke hupenda kusikia maneno yafuatayo; 'Unajua kwamba nakupenda,uko sahihi, usiku wa jana ulikuwa mzuri, nakupenda ukiwa hujapaka mak- up, ukweli ni kwamba huonekani kuwa mnene, nakupenda jinsi ulivyo, sielewi ila nitajaribu.

Share with Others