Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto imesema asilimia 40 ya wanawake wenye miaka 15 hadi 19 nchini
wameripotiwa kufanyiwa ukatili wa kimwili, huku asilimia 17 ya wanawake wenye miaka 15 hadi 49 wakifanyiwa ukatili wa
kingono.


Mkurugenzi msaidizi wa masuala ya Watoto SEBASTIAN KITIKU amesema takwimu hizo ni wale ambao wameripoti lakini wengine wananyamaza kimya bila kutoa taarifa wanapofanyiwa ukatili.

KITIKU amesema nusu ya wanawake waliolewa, asilimia 85 wamefanyiwa ukatili wa kimwili na asilimia 39 ukatili wa kiakili ambapo wanaofanya hayo ni wenza wao wa karibu na kiwango hicho ni kikubwa.


Ameongeza kuwa asilimia 54 ya wanawake ambao wamefanyiwa vitendo vya ukatili wamepata msaada kwa kwenda katika matibabu, kwenye Sheria pamoja na polisi huku wengine wakiamua kukaa nyumbani na kuendelea kupata maumivu.

 

Pamoja na hayo KITIKU amesisitiza kuwa ni vema waandishi wa habari  kuendelea kutoa elimu katika jamii kuhusu ukatili wa kijinsia kwa sababu wengi wao hawajui taratibu za kusaidiwa pale wanapopata matatizo hayo hasa kwa watu wao wa karibu.

Share with Others