Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amewatahadharisha wananchi wote waliopanga kufanya maandamano siku ya kesho kushinikiza Bunge kufanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad kuwa wasithubutu kufanya hivyo kwani watapigwa,watachakaa

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kamanda Muroto amesema kuwa kuna taarifa zilizolifikia Jeshi hilo  kuwa kuna vijana wa chama cha ACT- Wazalendo kwa kushirkiana na vyama vingine vya siasa vikiwemo vya NCCR MAGEUZI,CHAUMA,UPDP na vyama vingine vitatu ambavyo wanavijua wao.

''Wanaotarajia kufanya maandamano  siku ya jumanne tarehe 9/4/2019  waliyoyapa jina kuwa maandamano  ya amani  wakiwa na lengo la kulishinikiza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutekeleza kumshinikiza Spika wa Bunge kufuta azimio la Bunge la kutofanya kazi na CAG Pro Mussa Assad wakiingia barabarani watapigwa watachakaa,'' Muroto.

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na taarifa walizo nazo pamoja na taarifa zilizosambaa mtandaoni, Jeshi la Polisi Mkoani humo linapiga marufuku maandamano hayo kufanyika kwani hayatakuwa maandamano halali kwa kuwa hayana kibali.

Pia, amesema watambue kuwa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mhimili unaojitegemea na hautakiwa kuhojiwa nje ya Bunge kwani wanaohoji mipango na maazimio ya Bunge wamo ndani ya Bunge ambao ni Wabunge wenyewe walioteuliwa na wananchi  ili kuwawakilisha.
 

Share with Others