Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la FADHIL ABDALAH MKUNGUJA mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kijiji cha uchemi kata na tarafa ya milola wilaya ya Lindi ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na ISMAIL ISSA KHALIFA ambaye anashilikiliwa na jeshi la polisi. 

 

Tukio hilo limetokea tarehe sita mwezi huu majira ya saa sita usiku katika sherehe za unyago. Kamanda wa polisi Mkoani Lindi PRUDENSIA PROTAS amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi.

 

Awali akizungumzia tukio hilo ,HAWA AHAMDI ambaye anadaiwa kugombaniwa na kusababisha mauaji hayo amesema mumewake ISMAIL ISSA amefikia uamuzi huo baada ya kuhisi FADHIL ABDALAH anamahosiano naye ya kimapenzi.

 

Diwani wa kata ya Milola OMARI RASHID amesema kwa mujibu wa taarifa alizopatiwa na mtendaji wa kijiji zinaeleza mtuhumiwa ametoroka kijijini hapo na kwamba kwa kushirikiana na jeshi la polisi wanaendelea kufanya jitihada za kumtafuta.


 

Share with Others