Watu saba wamefariki dunia ikiwemo wafanyakazi watano wa Azam Media na wengine kujeruhuwa vibaya eneo la Malendi Singinda.

Ajali hiyo imetokea wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa hifadhi ya Burigi.

Kamanda wa Polisi Mkoani wa Singida, Sweetbert Njewike amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo

baadhi ya viongozi wa serikali wametoa salam za pole kwa familia akiwemo Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  ambapo Waziri wa Utalii na maliasili nchini Tanzania Dkt. Hamis Kigwangalla nae ameelezea kuguswa na vifo vya watu waliofariki katika jali hiyo leo.

.

"Moyo wangu umeshtuka na unatoa machozi ya damu kupata taarifa za kushtua na kusikitisha za ajali ya wafanyakazi wa Azam Media iliyotokea maeneo ya Malendi, Singida na kuchukua maisha ya 7 kati ya 10 waliokuwepo. Tunahangaika kutafuta usafiri wa haraka wa majeruhi hao 3," ameeleza Waziri Kigwangalla

Wafanyakazi wa Azam Media Limited waliofariki ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi, pamoja na madereva wa coaster na lori. Coaster ilikuwa na wafanyakazi 10 wa Azam wakielekea kwenye uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato.

 

Share with Others