Jumla ya barabara 376 zilizokuwa hazijasajiliwa kwenye mfumo wa wakala wa barabara Mijini na Vijijini TARURA katika Manispaa
ya Lindi zimeanza kuthibitishwa kuingia kwenye mfumo huo ikiwemo barabara inayoelekea Kipiye yenye urefu wa Km 1.5.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TARURA halmashauri ya manispaa ya Lindi INJINIA LUSEKELO MWAKYAMI wakati
akizungumza na Mashujaa FM mapema jana.

INJINIA MWAKYAMI amesema hivi sasa wanaendesha zoezi la sensa ya magari ambapo jumla ya barabara 23 zilizopo manispaa
ya Lindi zimeingia kwenye zoezi hilo ikiwa ni kipimo cha mipango yao ya utekelezaji wa barabara.

Share with Others