Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa serikali  itatoa shilingi bilioni moja kwaajili ya kuiwezesha Serengeti Boys.

Rais Magufuli amesema kuwa atatoa fedha hizo ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika kwa vijana AfconU17 yatakayofanyika nchini Tanzania mwezi Aprili mwaka huu.

Rais Magufuli amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Wizara ya Michezo kwa kuwa Timu ya Taifa Stars imemfurahisha sana baada ya kuipiga timu ya Uganda 3 bila.

Share with Others