CAG Prof Mussa Assad amesema kuwa NEC ilinunua mashine 5000 za bvr zisizokidhi vigezo mashine hizo  Ni kati ya 8000 zilizonunuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya usajili wa wapiga kura kwa njia ya kielektroniki

Pamoja na hayo Ripoti hiyo pia imebainisha  CHADEMA walinunua gari aina ya Nissan Patrol lenye thamani ya shilingi milioni 147.76 ambalo lilisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya Bodi ya Wadhamini ya chama hicho


Akiendelea kutoa ripoti CAG amesema wakati wa ukaguzi, alibaini matukio matatu ya udanganyifu wa Shilingi 321,377,067 ambayo yanahitaji uchunguzi Zaidi ambayo ni  Halmashauri ya Wilaya Mkuranga kiasi cha shilingi milioni 7,050,000 zilizokusanywa hazikupelekwa Benki kama utaratibu unavyoelekeza

Halmashauri ya Wilaya ya Tabora imebainika kufanya udanganyifu katika shilingi 270,540,067
ambapo yalifanyika mabadiliko ya hati ya malipo na orodha ya walipwaji kinyume cha utaratibu

Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge yalifanyika malipo ya Shilingi 43,787,000 kwa shughuli ambazo hazikufanyika(shughuli hewa)


Aidha Ripoti ya CAG imeeleza kuwa kuwapo kwa matukio haya ya ubadhirifu ni dalili kwamba mamlaka za Serikali za Mitaa zilizohusika hazichukui hatua stahiki za kubaini ubadhirifu kutokana na kutokuwa na mfumo madhubuti wa udhibiti wa ndani
 

CAG amesema 'Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma.
Tumewaalika wenyeviti wa kamati za Bunge (PAC na LAAC) lakini hawajaja hapa. Tutawapatia nakala hizi."

Share with Others