Daktari wa uzazi, Jan Karbaat anayeshutumiwa kwa kupandikiza mbegu zake za uzazi kwa wagonjwa bila ridhaa yao amethibitishwa kuwa baba wa watoto 49.

 

Vipimo vya vinasaba(DNA) vimefichua kuwa Daktari huyo aliyefariki dunia miaka miwili iliyopita aliwapa mimba Wanawake hao katika kliniki yake iliyopo eneo la Bijdorp, karibu na Rotterdam.

 

Mmoja wa watoto, kwa jina Joey, alisema hatimae amefunga ukurasa na baada ya miaka 11 ya uchunguzi sasa anajua Bwana Karbaat alikuwa ndiye baba yake.

 

Tim Bueters, Wakili aliyewawakilisha watoto hao 49, alisema ameridhishwa na matokeo ya kesi ya baada ya miaka 11 ya kutokuwa na uhakika.

 

Karbaat alipelekwa kwa mara ya kwanza Mahakamani mwaka 2017 na kikundi cha watoto baada ya kushuku kuwa alikuwa na uhusiano na Wazazi wao.

Share with Others