Elimu ya lishe bora bado ni changamoto kubwa katika maeneo mbalimbali wilayani Kilwa mkoani Lindi ambapo kwa kipindi cha
mwezi februari hadi mei watoto 10 wamegundulika kuwa na utapiamlo mkali.


Hayo yameelezwa na mratibu wa kitengo afya ya mama na mtoto INOSENSIA MANGOSONGO kwenye kikao cha kamati ya lishe
wilayani humo.

Baadhi ya wadau walioudhuria kikao hicho wameitaka halmashauri kuchukua hatua madhubuti kwa baadhi ya
wazalishaji na wafanyabiashara wa chumvi wanaouza chumvi isiyo na madini joto kwani nayo ni sababu kubwa ya kudumaa
kwa watoto.

Kwa upande wake Bwana afya wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa DKT. JEREMIA NDAIZEI amesema kwa kuliona hilo serikali inatoa madini joto kwa wazalishaji wadogowadogo wa chumvi ili kuhamasisha uwekaji wa madini hayo katika chumvi.

Share with Others