Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na Mafuta ya Taa hapa nchini zitakazoanza kutumika kuanziaTarehe 5 Juni 2019

Bei za rejareja kwa mafuta yanayoingia kupitia bandari ya Dar imeongezeka; Petroli imeongezeka kwa Tsh. 120/lita(5.35%), Dizeli imeongezeka kwa Tsh. 39/lita(1.81%) na Mafuta ya Taa imeongezeka kwa Tsh. 70/lita(3.34%)

Bei za rejareja kwa mafuta yaliyoingia nchini kupitia bandari ya Tanga imeongezeka kwa mafuta ya Petroli kwa Tsh. 105/lita(4.62%) na Dizeli imeongezeka kwa Tsh. 65/lita(2.92%). Bei za Mafuta ya Taa hazijabadilika kwa sababu hakuna shehena ya bidhaa hiyo iliyopokelewa kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi wa Mei 2019

Bei za rejareja kwa mafuta yaliyoingia nchini kupitia bandari ya Mtwara imeongezeka ambapo bei za Dizeli zimeongezeka kwa Tsh. 64/lita(2.84%). Bei za Petroli hazijabadilika kwa sababu hakuna shehena ya bidhaa hiyo iliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Mtwara kwa mwezi wa Mei 2019

Kwa kiasi kikubwa, mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la ndani kwa mafuta yaliyoingizwa nchini kupitia bandari yanatokana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji(BPS premiums)

Share with Others