WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,  Seleman Jafo amesema hajapendezwa na baadhi ya mikoa ambayo haikufikia malengo waliyowekewa ya kujenga viwanda si chini ya mia moja 100, kila mkoa kwa mwaka. 


Waziri JAFO ameyasema hayo jana Jijini Dodoma, wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa viwanda mia moja (100) kwa kila mkoa kwa kipindi kinachoishia desemba 2018.


Waziri JAFO amesema hakufurahishwa na mikoa hiyo ambayo haikufikia malengo hayo, na kuwapa muda hadi kufikia mwezi wa sita mwaka huu kuhakikisha wanafikia malengo waliyowekewa na serikali, ingawa hakuweza kuweka wazi mikoa hiyo ambayo haikufikia lengo.
 

Share with Others