Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudenciana Protas amethibitisha kukamatwa kwa Vijana watatu wanaodaiwa kuhusika na tukio la kuwapa biskuti zenye madawa ya kulevya abiria wawili waliopnda basi la BUTI LA ZUNGU kutoka Dar kwenda Mtwara na kufanikiwa kuwapora mali walizokuwa nazo ikiwemo fedha na laptop Vijana hao wamekamatwa kwenye Gesti ya Adela Lindi Mjini wakiwa na vitu mbalimbali ikiwemo Flash , kadi za benki, vyeti vya aina mbalimbali, simu na nguo za abiria waliopewa biskuti hizo na viatu huku akisema watuhumiwa hao  tayari wapo mikononi mwa Polisi wakiendelea kuhojiwa.Kaimu mganga mfawidhi Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi  Dkt.Idrisa Chande amesema kuwa afya za abiria hao zinaendelea kuimarika na bado hawajajua ni kiasi gani cha Dawa walilishwa.

Share with Others