Mkoa wa Lindi umeunda kamati 586 za ulinzi na usalama kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto.

Hayo yameelezwa leo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa(RCC)  Lindi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi.

Akizungumza kwenye kikao hicho kwaniaba ya katibu tawala wa mkoa( RAS ) wa  Lindi, katibu tawala msaidizi mipango na uratibu, Juhudi Mgallah alisema mkoa wa Lindi umeunda kamati hizo 586 ambazo, zitapambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kati ya hizo, kamati 6 niza halmashauri, 108 za kata na 476 ni vijiji.

Mgallah alisema mashauri 1827 yanayohusu migogoro ya kifamilia yalipelekwa na kufika katika ofisi za ustawi wa jamii. Huku akieleza kwamba mashauri 418 yalihusu ndoa, 879 ya matunzo ya watoto na watoto nje ya ndoa  ni 530.

Sanjari na kuundwa kamati za ulinzi na usalama, amesema mkoa huo umeweza kuunda mabaraza ya wazee 241 ya ngazi ya vijiji na mitaa, 98 ya ngazi ya kata na 6 niya ngazi ya halmashauri.

Pamoja na hayo amebainisha kwamba wazee 51,139 ambao ni sawa na 77% ya idadi ya wazee 66,072 ametambuliwa. Ambapo wazee 15,357 kati hao waliotambuliwa wamepewa vitambulisho vya msamaha. MWISHO.

Share with Others