Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba amesema katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya Plastiki ifikapo Mwezi June Mosi Mwaka huu halikuja ghafla na wadau wote walishirikishwa.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa mifuko ya Plastiki wakiwemo wazalishaji Waziri Makamba amesema katazo hilo halitahusisha vifungashio vya Plastiki.

Waziri Makamba amesema katazo hilo ni la kisheria na halina athari zozote kwa uchumi wa nchi na badala yake kutakuwa na fursa mpya ya kutengeneza mifuko mbadala ambayo haina athari kwa mazingira.

Katika hatua nyingine Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Josephat Kakunda amesema zipo athari kubwa za kiafya ikiwemo kupata kansa iwapo mifuko ya Plastiki itatumika kufunikia Chakula ili kisipoe ingawa watu wengi wekuwa wakiitumia mifuko hiyo kufunikia Chakula.

Share with Others