Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. JOHN POMBE MAGUFULI amewazawadia kila mchezaji wa Taifa Stars zawadi ya kiwanja Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma.

Rais Magufuli amesema kuwa amewapa zawadi hiyo kwa niaba ya Watanzania kwasababu wamewafurahisha katika mchezo wa jana.

"Mimi kama mimi sina kitu, ila kwa niaba ya Watanzania sisi tunawapa zawadi za kiwanja kwa kila mmoja,Hassan Mwakinyo na mwalimu wako, Peter Tino na Ndugu Tenga, kila mmoja apate kiwanja chake, naomba Waziri Mkuu naomba usimamie hili. Sasa ukishapata kiwanja ukiamua kukiuza shauri yako, sisi kama Watanzania hiyo ndio shukrani yetu," Amesema Rais Magufuli Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Share with Others