Halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi imejipanga kuboresha miundombinu ya sekta ya uvuvi ikiwemo ujenzi wa vizimba, kuanzishwa kwa minada ya samaki na ujenzi wa soko la kisasa katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Kivinje.

 

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo RENATUS MCHAU wakati akizungumza na Mashujaa FM ambapo amesema sekta ya uvuvi inasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukua kwa uchumi wa Halmashauri hiyo hivyo lazima iboreshwe.

 

MCHAU amesema maboresho hayo yataongeza makusanyo ya ushuru unaotokana na uvuvi, hadi kufikia shillingi milioni 20 kwa
wiki ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo makusanyo yalikuwa haizidi milioni tano.

Share with Others