Inaripotiwa kuwa zaidi ya kondoo 12 wameandikishwa katika shule ya msingi nchini Ufaransa kama wanafunzi baada ya hofu kuwa shule hiyo inaweza kufungwa kwa kukosa waalimu.

 

Takriban kondoo 50 waliletwa katika shule hiyo na mkulima mmoja nchini humo mapema mwezi huu na 15 kati yao walisajiliwa baada ya kuonyesha vyeti vya kuzaliwa.

 

Hatua hii ilichukuliwa baada ya Shule ya Jules Ferry iliyopo kwenye kijiji cha Crêts-en-Belledonne,kijiji cha watu chini ya 4,000, kuripotiwa kuwa madarasa yake 11 ingefungwa baada ya idadi ya wanafunzi kushuka kutoka 266 hadi 261.

Share with Others