Licha ya kuwepo taarifa za ugonjwa wa DENGI katika mkoa wa DARES SALAAM na mikoa mingine hapa nchini, imeelezwa kuwa katika mkoa wa Lindi hakuna taarifa ya kupatikana kwa Mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo.

Taarifa hiyo imetolewa na Dkt. ALEX DISMASI HAMISI ambaye ni mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Lindi wakati akizungumza na mashujaa FM kuhusu ugonjwa wa DENGI. Dokta ALEX amesema ugonjwa wa DENGI unasambazwa na Mbu
ambao wanakaa katika maji masafi na maji machafu yaliyotuama.

Mashujaa FM imezungumza na baadhi ya wakazi wa wanaspaa ya Lindi ili kutaka kujua namna wanavyojikinga na ugonjwa wa DENGI ambapo wamesema wanajikinga kwa kuondoa uchafu na mazalia ya Mbu katika maeneo yao, huku wengine wakisema hawaufahamu ugonjwa huo.

Share with Others