Mkoa wa Lindi umeshika nafasi ya kwanza kitaifa kwa ufaulu katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019 ikiwa imepanda kutoka nafasi ya pili kwa matokeo ya mwaka 2018 

 

Afisa elimu mkoa wa Lindi Vicent Kayombo amesema kilichochangia ufaulu kupanda ni kutokana na ufundishaji kwa walimu, msukumo wa wazazi kwa wanafunzi na viongozi kusimamia dhamana waliyopewa 

 

Amesema kwa mkoa wa Lindi wana sekondari 9 ambapo kote huko hakuna mwanafunzi aliyefeli huku shule ya Sekondari Nyangao ikiongoza kwa kufanya vizuri kimkoa

 

Aidha amesema kuwa katika mkoa mzima ni wanaafunzi 6 pekee waliopata division 4 na kwamba Wilaya inayoongoza ni wilaya ya Nachigwea ikifuatiwa na Ruagwa, Lindi vijijini, Kilwa, Liwale huku Lindi mjini ikikamata nafasi ya mwisho kimkoa 

 

Pia ameipongeza Mashujaa Fm kwa kuchangia ufaulu katika matokeo hayo kupitia vipindi vyake 

 

 

 

Share with Others