Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mkoani wa Lindi wameitaka serikali ya mkoa huo kuiachia Halmashauri hiyo jukumu la kusimamia taratibu zote za mauzo ya zao la ufuta.


Hayo yameelezwa na madiwani hao katika kikao cha baraza la madiwani ambapo wamesema halmashauri hiyo ikiachiwa jukumu la kusimamia taratibu zote za uuzaji wa zao hilo ikiwemo minada, tenda na mambo mengine itaweza kusimamia vyema mapato yake.

Mwanasheria wa halmashauri hiyo JOFREY JAFARI amewatoa hofu Madiwani hao, kwa kueleza kuwa hakuna mapato yanayopotea hata kama mkoa utaendelea kusimamia uuzaji wa zao hilo, hivyo ni vyema wakashirikiana katika kusimamia kwa manufaa ya wote.

 

Share with Others