Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kisarawe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi Jokate Mwegelo na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar es salaam (Mhandisi) Ally Maganga wametemblea maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo kwa lengo la kujenga uelewa wa Pamoja wa shughuli za uchimbaji Madini ya Kaolin katika Wilaya hiyo

Katika Ziara hiyo, Kamati imeweza kubainisha maeneo rafiki ya uwekezaji wa shughuli za madini ambao utaepuka muingiliano na mgongano wa shughuli hizo na makazi ya watu ikiwepo kuepuka uchafuzi wa Mazingira. Mtizamo huo unaenda sambamba na maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo (Mb) aliyoyatoa katika Ziara yake mwishoni mwa mwezi, Juni mwaka huu

Share with Others