Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara kuanzia Aprili 2 hadi April 4

Katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara na ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata (Km 50)

Pia ataweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha kubangua korosho cha Yalin kilichopo Msijute na ataweka pia jiwe la msingi katika chuo cha ualimu cha Kitangali

Hii ni ziara ya pili kwa Rais Magufuli kutembelea Mkoa wa Mtwara tangu alipoapishwa kuwa Rais mwaka 2015, ambapo safari hii anatarajiwa kuzunguka katika Wilaya zote za Mkoa huu

Share with Others