Jaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Latifa Mansour amekubaliana na uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge Joshua Nassari (Arumeru Mashariki). 

Jaji Mansour ametumia dakika  44 kusoma maelezo yaliyomweka katika wakati mgumu Nassari. 

Machi 14, 2019 Ndugai aliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) barua akiieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa. 

Spika Ndugai aliitaja mikutano hiyo kuwa ni wa 12 ulioanza Septemba 4 hadi 14; Novemba 6 hadi 16, 2018 na wa Januari 29 hadi 9. 

Baada ya uamuzi huo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amemuagiza Nassari kuzungumza na wananchi na wanachama wa jimbo lake kuwaeleza kilichotokea. 

Akisoma uamuzi wake leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji huyo  ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.
 

Share with Others