Mahakama  hiyo ya Juu nchini humo imehalalisha ushoga  kwa kuondoa kifungu cha sheria kilichokuwa kikikataza vitendo hivyo

Mawakili waliokuwa wakitaka ushoga uhalalishwe walisimamia hoja ya kwamba, sheria inayopinga mapenzi hayo ya jinsia moja baina ya wanaume kwa wanaume ni ya Kikoloni hivyo lazima iondolewe.

Awali Shauri hilo lilianza kusikilizwa tangu mwaka 2013 ambapo Mahakama ilikataa kuhalalisha ushoga lakini watetezi wa haki za mashoga walikata rufaa juu ya maamuzi hayo.

Miaka iliyopita Nchini India kufanya ushoga ilikuwa ni kosa la jinai.
 

Share with Others