Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Phillip Mangula ametoa onyo kwa watumishi wa serikali wanaotarajia kuwania nafasi za uongozi katika chama hicho kuacha mara moja, na badala yake watumie muda wao mwingi katika kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesema na makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Phillip Mangula wakati akizungumza na viongozi wa chama, na serikali na baadhi ya wazee wilayani mkuranga mkoa wa Pwani.

Mangula pia amewataka viongozi kuacha tabia ya kulalamika mbele ya wananchi na badala yake kutafuta majibu sahihi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Katika kikao hicho katibu tawala msaidizi mkoa wa Pwani, Shangwe Twamala akiwasilisha taarifa ya ukusanyaji wa zao la korosho ,usafirishaji na namna malipo yananvyoendela amesema zaidi ya shlingi bilioni 45 zimelipwa kwa wakulima.

Share with Others