Walimu wa shule ya sekondari Kipaumbele wilayani Nachingwea mkoani Lindi wameshukuru na kupongeza jitihada za Mashujaa
Fm katika kuchangia maendeleo ya elimu wilayani humo kwa kutoa hamasa kwa wanafunzi kwa kutumia maneno na
vitendo .


Wameeleza hayo mara baada ya Mashujaa Fm kutembelea shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha Nne
wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya sekondari tarehe 4/11/2019.


Aidha Wameeleza kuwa, kwa muda mrefu shule hiyo ikikosa wadau wa elimu ambao wanaweza kuzungumza na wanafunzi kwa lengo la kuwapa hamasa katika mitihani na masomo yao.

Sambamba na hamasa kwa njia ya kuzungumza na wanafunzi hao lakini pia Mashujaa fm imewagawia wanafunzi wa kidato cha nne baadhi ya vifaa kwaajili ya maandilizi ya mitihani yao.

Share with Others