Serikali imeahidi kutatua Mgogoro wa ardhi uliopo kati ya kambi ya jeshi la MajiMaji na JKT dhidi ya wakazi wa kata ya Kilimanihewa na Mchonda wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.


Ahadi hiyo imetolewa leo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa DKT HUSSEIN MWINYI wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kilimanihewa, Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea na viongozi wa vikosi vyote viwili ambavyo vimeingia katika mgogoro na wananchi hao.


Waziri MWINYI amesema hayo yamefikiwa baada ya Kuzipitia ripoti zilizotolewa na tume zilizoundwa kwaajili ya kutatua mgogoro huo ulioanza mwaka 1978.


Akifafanua Suala hilo Waziri MWINYI amesema anautambua mgogoro huo na kupitia tume tatu ambazo ziliundwa kwaajili ya kuutatua ikiwemo tume ya wilaya, mkoa na ya Kamishna wa ardhi wa kanda baadhi ya ripoti bado hajazipata, hivyo akizipata atalifanyia kazi.


Aidha Waziri MWINYI ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kutoruhusu Malipo ya korosho zinazodhaniwa kuwa zimechukuliwa na baadhi ya wanajeshi kutoka kwa wananchi waliojenga ndani ya kambi za jeshi ambazo awali ilionesha kuwa zitamilikiwa na kikosi, lakini baadae ikaonekana inabidi zilipwe kwenye akaunti binafsi.

Share with Others