Wajasiliamali Mkoani Lindi wameaswa kuendelea kujitangaza pamoja na kubuni vifungashio vyenye tija zaidi vitakavyoongeza thamani ya bidhaa wanazozizalisha.


 Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa mhe HASHIM MGANDILWA ameyasema hayo wakati akifunga jukwaa la fursa za biashara na uwekezaji kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Lindi ,lililodumu kwa muda wa siku tatu mkoani humo.


Aidha amezitaka taasisi za serikali ambazo zinahusika na wajasiliamali kufikiria amna ya kuanzisha vituo vya utoaji wa taarifa za masoko zitakazowasaidia wajasiliamali kujua ni wapi na wakati gani ambao wanaweza kupata soko la uhakika la bidhaa anayoizalisha.


MECKTIDIS MICHAEL ni mmoja kati ya wajasiliamali walioshiriki katika jukwaa hilo ,kwa upande wake ameishukuru kampuni ya Tsn kwa kushirikiana na mkoa wa Lindi kufanyika kwa jukwaa la fursa huku akiiomba serikali ya mkoa kutenga neo litakalowakutanisha ili kuuza bidhaa zao .


Ufungwaji wa jukwaa hilo umeambatana na utoaji wa yeti vya kutambua ushiriki wao kwa wajasiliamali na taasisi mbalimbali ambazo zimeshiriki .

Share with Others