Mtu mmoja ambaye alithibitishwa kuwa na maambukizi ya #HantaVirus amefariki dunia akiwa kwenye basi katika Jimbo ya Yunnan. Abiria wengine 32 waliokuwa kwenye basi hilo wamefanyiwa vipimo kuona kama wameathirikaKifo hicho kimekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kutokana na wengi kukifananisha na #CoronaVirus, ambayo pia ilianzia China

Wataalam wa afya wameeleza kwamba #HantaVirus husambazwa na Panya wenye Virusi hivyo na ni vigumu kwa watu kuambukizana

Kwa mujibu wa Kituo cha kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekani (CDC), mtu anaweza kuambukizwa pale anaposhika macho, pua au mdomo wake baada ya kushika haja, mkojo au mate wa Panya

Share with Others