Mwenyekiti na wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Namatula A wilayani Nachingwea mkoani Lindi, wametuhumiwa kutotumia ipasavyo Mashine ya Kielektroniki ya ukusanyaji mapato ( EFD) katika chanzo cha machimbo ya mchanga kijijini hapo.


Wakizungumza na Mashujaa Fm wakazi hao wameeleza kuwa mwanzo ukusanyaji wa mapato ulikuwa sio nzuri sana ila waliweza kufanikisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa zahanati na kwa sasa halmashauri ya wilaya imepeleka mashine ya EFD lakini haitumiki sawa sawa. 

 

Akijibia tuhuma hizo mwenyekiti wa kijiji cha Namatula A, ANAFI SAIDI amekanusha taarifa hizo kwa kueleza kuwa wamekuwa na utaratibu mpya wa kukusanya tozo hizo pale tu mteja anapo maliza tripu ya mwisho ya mchanga aliouhitaji.


Aidha ANAFI amewaomba wakazi wa kijiji hiko kuachana na mtazamo usio sahihi kwani lengo la serikali ya kijiji ni kujenga na kufanikisha shughuli za maendeleo.
 

Share with Others