Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne, kidato cha pili na darasa la nne kwa mwaka 2019 ambapo kwa kidato cha nne NECTA imesema Watahiniwa 340,914 sawa na 80.65% wamefaulu kati ya Watahiniwa 422,722 waliofanya Mtihani hii ikiwa ni sawa na ongezeko la 1.38 asilimia ikilinganishwa na watahiniwa 284,126  sawa na 79.27 asilimia waliofaulu Mtihani huo 2018.

 

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo na Katibu Mtendaji NECTA, Dk Charles Msonde amesema ufaulu katika mtihani wa upimaji wa Darasa la nne umeongezeka kwa 26.21 asilimia ambapo watahiniwa 1,531,120 kati ya watahiniwa 1,665,863 wamepata alama A,B,C na D ikilinganishwa na wanafunzi 1,213,132 waliofaulu mwaka 2018.

 

Aidha katika mtihani wa upimaji kidato cha pili, Dk Msonde amesema wanafunzi 514,251 sawa na 90.04 asilimia kati ya wanafunzi 571,137 wamefanya vizuri katika mtihani huo na kuwawezesha kuingia kidato cha tatu

 

 

Share with Others