Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo (FAO) limeonya kwamba nzige walioivamia Ethiopia, Kenya na Somalia sasa ni wimbi kubwa kuwahi kushuhudiwa hivi karibuni na lisipodhibitiwa kuna uwezekano wa kusambaa katika nchi nyingine za Afrika Mashariki

Ethiopia, Kenya na Somalia zinapitia wakati mgumu kukabiliana na makundi ya nzige ambako hakujawahi kutokea hapo kabla kunakoathiri mazao ya kilimo, limesema shirika la FAO

Shirika hilo linahofia kwamba idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo Juni mwaka huu

Ethiopia na Somalia hazijawahi kushuhudia nzige wa aina hiyo kwa kipindi cha miaka 25 huku Kenya ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 70, shirika la FAO limesema hivyo mapema wiki hii

Sudani Kusini na Uganda pia zipo katika hatari ya kuingiliwa na nzige hao ambao wanaendelea kuongezeka na kusambaa

"Kasi ya kusambaa kwa nzige hao na kiwango ambacho wanavamia maeneo siyo kawaida kiasi cha kuwa changamoto hata kwa mamlaka za eneo na za kitaifa," kulingana na FAO

Chaguo pekee lililosalia kukabiliana na nzige hao ni kutumia ndege ambazo zinanyunyiza dawa ya kuua wadudu

Nzige wanaweza kusafiri umbali wa kilomita 150 (maili 93) kwa siku na kila nzige mkubwa anaweza kula chakula kiasi kikubwa tu cha chakula kwa siku

Kundi la nzige kama hivyo mjini Paris linaweza kula kiasi sawa cha chakula kinachoweza kuliwa na nusu idadi ya watu wote Ufaransa kwa siku moja, kulingana taarifa za maelezo za FAO

Share with Others