Spika wa Bunge Job Ndugai amesema taarifa ya kukaguliwa ofisi ya CAG tayari ameshaipitia ila kuna mambo kadhaa ya kuweka sawa.

Akizungumza leo Bungeni amesema kuwa mambo hayo ni kuipeleka kamati ya PAC kisha watairudisha kwake na kuitolea tamko rasmi.

"Ningependa kuwajulisha juu ya taarifa ya  ukaguzi wa ofisi ya CAG kwa mwaka fedha unaoshia Juni, 2018, hesabu za CAG zinapaswa kukaguliwa walau mara moja kwa mwaka, PAC inajukumu la kukagua ofisi hiyo, kazi imeshafanyika na tumeletewa  taarifa," amesema.


Ameendelea kwa kusema kuwa, "Taarifa ya kukaguliwa ofisi ya CAG, nimeshaipitia kuna mambo, lakini kiutaratibu nimeshaipeleka PAC na wakishamaliza uchambuzi watawasilisha kwangu, niwataarifu kwenye masuala ya ukaguzi hakuna anayebaki kila watu wanawakagua wenzao,".


 

Share with Others