Jeshi la polisi wilayani Liwale limesema licha ya kuwepo kwa matukio mengi yanayoripotiwa ya wanafunzi wa kike kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, lakini inawawia vigumu kuyafikisha mahakamani kwa kukosa ushirikiano kutoka kwa jamii.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Liwale Edward Malogo wakati akiongea na Mashujaa FM ambapo ametoa wito kwa jamii kuacha kushirikiana na wanafunzi katika masuala hayo na badala yake walisaidie Jeshi hilo kufichua wahusika.

MALOGO amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa wazazi na walezi wilayani humo kuripoti matukio ya tabia zisizoridhisha kwa watoto wao wa kike ambao wamekuwa wakitoroka nyumbani nyakati za usiku na kwenda kwa wanaume.

Hayo yanaendelea kutokea huku mkowa wa Lindi ukiendelea na kampeni ya kupinga mimba za utotoni yenye kauli mbiu isemayo
'Tumsaidie Akue, Asome, Mimba baadaye', inayolenga kupinga mimba za utotoni.

Share with Others